Baada ya msanii kutoka Cash Money Records kuachana na aliyekuwa mpenzi wake wa miaka 12, Safaree Samuels kumekuwa na headlines nyingi za ugomvi kati ya wawili hao. Miezi michache iliyopita Nicki Minaj na Safaree Samuels walishambuliana kwenye mitandao ya kijamii huku Safaree akidai Nicki alianza mahusiano na Meek Mill wakati bado wapo pamoja… Safaree karudi tena na time hii amesema anaenda moja kwa moja Mahakamani kudai kilicho chake!
Safaree Samuels & Nicki Minaj.
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, Safraree amepeleka madai yake Mahakamani na kutaka asilimia yake ya pesa kutoka kwenye Album tatu za Nicki Minaj: The Pinkprint, Pink Friday na Pink Friday: Roman Reloaded, huku akidai pesa kubwa zaidi ya pesa kwenye mauzo yaliopatikana kwenye single 3 kubwa za Nicki, Only aliyomshirikisha Chris Brown, Drake na Lil Wayne, Flawless (Remix) wimbo aliofanya na Beyonce pamoja na share yake kwenye wimbo wa Feeling Myself aliomshirikisha Beyonce Knowles.
Nicki Minaj & Meek Mill.
Safaree ambaye pia ni rapper na mtunzi wa nyimbo amedai kuwa amekuwa chombo cha muhimu sana kwenye uandishi na utengenezaji muziki wa Nicki Minaj, na pia Nicki alimchaguwa kuwa executive producer wake kwenye Album zake mbili, Pink Friday na Pink Friday: Roman Reloaded.
Kingine alichogusia Safaree kwa mujibu wa TMZ ni ushahidi wa videos za yeye na Nicki wakiwa studio wanafanya kazi, na footage tofauti kutoka kwenye studio nyingine walizokuwa wanaenda kufanya kazi pamoja.
Nicki Minaj & Safaree Samuels.
>>>” kila ikifika wakati wa kuandika mistari na kutengeneza muziki, ilikuwa mimi na yeye. Alikuwa hafanyi mwenyewe, ilikuwa ni mimi na yeye. Usininyime credit kwa kile nilichokufanyia…“<<< Safaree aliwahi kukiambia kipindi cha The Breakfast Club mwanzo wa mwaka huu
Comments
Post a Comment