Hiki ndicho kilichomkuta Neyma baada ya kumkabidhi refa zawadi ya jezi ....

Mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil Neymarameingia katika headlines baada ya kumalizika kwa mchezo kati ya timu yake ya taifa ya Brazildhidi ya Peru, mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2018 Urusi lakini Brazil iliibuka na ushindi wa goli 3-0 magoli ambayo yalifungwa na Douglas CostaRenato Augusto, na Felipe Luis.
Baada ya mechi kumalizika Neymar aliona ni vyema kwenda kumpa zawadi ya jezi muamuzi wa mechi hiyo Jose Buitrago kutokeaColombia lakini muamuzi aliikataa jezi yaNeymar kitendo ambacho kinatafsirika kama muamuzi huyo aliogopa kuchukua kwa sababu huenda angeonekana kapendelea, lakini utamaduni wa kupata saini au jezi ya staa kwa watu wa nje ya Afrika ni kitu muhimu sana na wanaheshimu hivyo wengi walishangazwa kuona kapotezea kumbukumbu muhimu

https://youtu.be/86umdJZ_tkE

Comments